Issa Shivji na Deus Kibamba, (1999)

Issa Shivji na Deus Kibamba, (1999) . MWONGOZO WA HAKI ZA ARDHI KWA WANANCHI WA TANZANIA; Uzoefu wa Haki za Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro.

Makala zilizomo katika mwongozo huu awali zilitayarishwa na kuwasilishwa katika warsha ya siku tano ya kufundisha wawezeshaji wa haki za ardhi iliyoandaliwa na HAKIARDHI kwa kushirikiana na mradi wa maendeleo ya wafugaji wa Ngorongoro (ERETO) na kufanyika Arusha kuanzia Tarehe 17 – 21 Januari 2000 chini ya ufadhili wa Shirika la maendeleo la watu wa Denmark (DANIADA). Mwishoni mwa warsha hiyo ilipendekezwa kuwa kuchapishwe mwongozo wa ufundishaji wawezeshaji kutokana na mada, mijadala, na mapendekezo yaliyojitokeza katika warsha hiyo. Pia ilipendekezwa kuwa mwongozo huu utumike kama Kiongozi cha Mafunzo ya siku zijazo kuhusu haki za ardhi na za binadamu kwa ujumla sio tu katika eneo la Ngorongoro bali pia kwingineko nchini.

Issa Shivji.G ni Profess wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mhadhiri mahiri ailyetoa machapicho mengi juu ya sheria za kazi, falsfa ya sheria, masuala ya katiba na sheria za ardhi. Issa Shivji alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuchunguza maswala ya ardhi (1991 -92) pia ni mmoja wa wakurugenzi na mwanachama wa HAKIARDHI.

Deus Kibamba ni mwanaharakati anayeibukia katika masuala ya utafit na utetezi wa Haki za Binadamu na Ardhi. Ana shahada ya kwanza (BA) katika sayansi za jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili (MA) katika fani ya Siasa ya Uchumi na maendeleo katika chuo kikuu cha Sheffield, Uingereza. Kibamba ametoa mawazo yake mara nyingi katika makala mbalimbali zikiwemo zilizochapishwa kwen vitabu, majarida, na magazeti ya hapa nchini. Ndugu Kibamba aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mpango katika Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi (HAKIARDHI).

NB; No more copies available