By Issa Shivji & Wilbert Kapinga (1998)

HAKI ZA WAMASAI WAISHIO HIFADHI YA NGORONGORO (Issa Shivji G. na Wibert Kapinga) 1998
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro linafikiria kuwa “la nane katika maajabu ya Dunia” na ni kivutio kikubwa sana cha utalii. Eneo hili pia ni makazi ya wafugaji wa Kimaasai wapatao 40,000, ambao toka mwaka 1958,n walipohamishiwa eneo hilo na serikali ya kikoloni, wamekuwa wakipigania haki zao za kisiasa na kiraia.
Haki za wamasai washio katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Tanzania ni uchambuzi wa utangulizi juu ya haki za wamasai na wakazi wa wengine waishio katika eneo la hifadhi. Haki zinazochunguzwa ni zile zinazohusiana na Uhuru wa kujishirikisha na mtu kwenda atakako ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kitabu hiki kinaziweka bayana haki zinazominywa, za wakazi wa eneo hili, hasa kuhusiana na mali, njia za kujikimu kimaisha, na ushirikishwaji katika maamuzi yenye athari katika maisha yao. Kitabu hiki kinatoa tathmini ya nguvu za kisheria na hali halisi ya utawala wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Nguvu hizi zinatazamwa kwa kuangalia na kuzingatia misingi ya utawala wa sheria na kidemokrasia. Hoja wanayotoa Waandishi wa kitabu hiki ni kuwa mipaka waliyowekewa Wamaasai na Mamlaka inaweza ikahalalishwa endapo tu Wamaasai na wakazi wengine walishirikishwa na kushauriwa kikamilifu katika mwenendo mzima wa kutoa maamuzi.
Waandishi wanapendekeza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro haina budi kuundwa upya. Jambo la muhimu na la kuzingatia katika uundwaji huu mpya ni kutoa fursa ifaayo kwaajili ya uwakilishi na ushirikishi wa Wamaasai na wakazi wengine katika muamua ni nujia ipi bora ya uhifadhi na kuendeleza maliasili hii muhimu.

Issa Shivji.G ni Profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mhadhiri mahiri ailyetoa machapicho mengi juu ya sheria za kazi, falsfa ya sheria, masuala ya katiba na sheria za ardhi. Issa Shivji alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuchunguza maswala ya ardhi (1991 -92) pia ni mmoja wa wakurugenzi na mwanachama wa HAKIARDHI. Pia ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Wilbert B. Kapinga hadi mwaka 1997 alikuwa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria na Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amechapisha makala mbalimbali juu ya sheria za kazi, sheria za ardhi, haki za binadamu, elimu ya sheria na taaluma ya sheria na sera za Umma. Dk. Kapinga pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa HAKIARDHI. Yeye ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.